Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida (Aliyeketi katikati), pamoja na Katibu Mkuu Hazina Dkt. Natu El-Maamry na Katibu Mkuu Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba, wakiwa katika mkutano wa Africa Energy Summit – mkutano mkubwa unaowakutanisha wakuu wa nchi zaidi ya 20, viongozi wa Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika, wadau wa maendeleo na wataalamu mbalimbali wa sekta ya nishati.