Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DKT. KIDA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA SAMAKI JIJINI MWANZA CHA VICTORIA PERCH LIMITED


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida ametembelea na kujionea maendeleo ya kiwanda cha kuchakata samaki jijini Mwanza (Victoria Perch Limited) ambacho uwekezaji wake ni zaidi ya dola milioni 3 za kimarekani (Zaidi ya bilioni 7 za Tanzania).

Dk. Kida yupo jijini Mwanza katika ziara ya kikazi ambako ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Gilead Teri na maofisa wengine wa TIC katika muendelezo wa kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani.