Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA KUPITIA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb.), akihutubia katika kongamano la Thought Leadership on China - Africa Trade and Investment Forum lililoandaliwa na Benki ya Viwanda na Biashara ya China, jijini Beijing.

Kongamano hilo ni mingoni mwa shughuli mbalimbali zinazofanyika pembezoni mwa mkutano wa FOCAC, na limelenga kuhamasisha uwekezaji katika sekta za miundombinu, madini, nishati na kilimo kwenye nchi za Afrika.

Aidha, Kongamano hilo limehudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Nchi walioalikwa, Mawaziri na Maafisa Waandamizi pamoja na Wawekezaji na Taasisi za Kifedha za kimataifa.

Mheshimiwa Prof. Mkumbo amepata nafasi ya kueleza kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini, huku ujumbe wa Tanzania ukipata fursa ya kukutana na wawekezaji wakubwa katika sekta za miundombinu, madini, nishati na kilimo.