Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO AKUTANA NA MKURUGENZI WA GATSBY, WAJADILI KUIMARISHA USHIRIKIANO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, Juni 3, 2025, alikutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Gatsby, Bw. Justin Highstead, jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo, likiwemo Shirika la Gatsby.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Prof. Mkumbo alipongeza mchango wa Shirika la Gatsby katika kusukuma ajenda za maendeleo nchini, hususani katika maboresho yanayoendelea kwenye sekta mbalimbali.

Kwa upande wake, Bw. Highstead alieleza kuwa shirika lake litaendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa mchango wake katika kujenga uwezo na kushirikiana katika kutekeleza baadhi ya mikakati ya maendeleo.